Wednesday, March 20, 2013

Maendeleo hayana mipaka ya vyama.

 Rais Jakaya Kikwete akiwa na mbunge wa Ubungo John Mnyika (chadema) wakati wa uzinduzi wa daraja la Golani lililo kata ya Ubungo Kimara Suka.

 Rais Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kimara waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wa Daraja linalounganisha vijiji.

 Uzinduzi wa daraja, John Mnyika kwa mbaali akionekana kujawa furaha kutokana na hatua hiyo ya kupigiwa mfano.

Kama nilivyosema maendeleo hayana mipaka ya vyama. Hapa zinaonekana bendera za vyama vitatu CCM, CHADEMA na CUF wakati Rais akizungumza na wananchi wa Kimara, mbali ya mambpo mengine Rais Kikwete alizungumzia shida ya maji suala lililozua mtafaruku bungeni na siku chache Serikali ilitoa agizo la kusitisha maandamano ya John Mnyika kudai maji. Kikwete amesema atalishughulikia tatizo hilo kabla hajaondoka madarakani.

picha kwa hisani ya Mjengwa website.

No comments:

Post a Comment