Waziri wa afya wa Afrika Kusini Amesema kuwa zaidi ya
asili mia 28% ya wasichana wa shule wameambukizwa virusi vya Ukimwi,
ikilinganishwa na asili mia 4% tu ya vijana wa shule.
Hii
ameelezea ni kutokana pakubwa na kuongezeka kwa mababa sukari au kwa jina lingine,
*fataki*, ( Wazee wanao tembea na wasichana wadogo kwa umri).
Waziri Aaron Motsoaledi amesema kuwa wamepata ushahidi kuwa
wasichana wengi wamejiingiza katika mapenzi na wazee waliowazidi ki umri badala
ya kuwa na vijana wa rika lao.
Takwimu za punde zaidi zimeonyesha kuwa asili
mia kumi ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya HIV. Nchi hiyo imekuwa
na mradi wa kuvuma zaidi wa kutoa dawa za kukabili makali ya virusi hivyo vya
HIV , ARV tangu rais Jacob Zuma alipomteua bwana Motsoaledi kuongoza wizara
hiyo ya afya yapata miaka minee iliyopita.
'Kupotosha
watoto'
Waziri
huyo pia aliongeza kuwa zaidi ya wasichana 94,000 walipata mimba katika mwaka
wa 2001 and kati yao 77, 000 walilazimika kuavya
mimba hizo katika kliniki za serikali, kwa mujibu wa taarfa katika magazeti ya Soweto .
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara katika mji wa Carolina ,
mkoa wa Mpumalanga , bwana Motsoaledi alisema
kuwa idadi hiyo kubwa ya wasichana wanaoharibiwa maisha yao
''inanivunja moyo sana ''.
''Lazima tuchukue hatua dhidi ya mababa sukari
hawa kwasababu wanaangamiza vizazi vyetu''.
Mwaka
uliopita zaidi ya watu 260,000 wanaoishi na Ukimwi walifariki ikiwa ni takriban
nusu ya watu wote waliofariki katika nchi hiyo.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment