RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) amewataka wadau wa mchezo huo kuwa watulivu kwa vile tofauti
zilizojitokeza kati ya Shirikisho na Serikali zitamalizwa kwa taratibu za mpira
wa miguu. Amesema nia ya TFF ni kuhakikisha Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA) haliifungii Tanzania
kwani tayari Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella
Mukangara alishaahidi kuwepo kikao kati yake na viongozi wa TFF
kitakachofanyika Jumanne
(Machi 19 mwaka huu).“Suluhu itapatikana
kwa mazungumzo kati ya Wizara na TFF. Naamini suala hili tutalimaliza baada ya
kikao cha Machi 19 ambacho kimepangwa na Waziri kutokana na maombi ya TFF,”
amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa tatizo lilianzia kwenye mchakato wa
uchaguzi ambao umesimamishwa na FIFA. FIFA ilisimamisha Mkutano Mkuu wa
uchaguzi baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika, na yenyewe
kuahidi kutuma ujumbe wa kushughulikia suala hilo .
Rais Tenga amesema lisingetokea
tatizo hilo , TFF
tayari ilishaitisha Mkutano Mkuu ambao ungefuatiwa na uchaguzi. Lakini kwa vile
FIFA ndiyo iliyosimamisha mkutano huo, TFF inalazimika kusubiri hadi FIFA
itakaposhughulikia suala hilo
na kutoa maelekezo ikiwemo lini mkutano ufanyike.
Amesema kwa kuamini tatizo hilo litamalizwa ndani ndiyo maana TFF hadi sasa
haijapeleka FIFA maagizo ya Waziri Dk. Fenella ya kutengua marekebisho ya
Katiba ya TFF ya mwaka 2012, kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba na
Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, kwani ingefanya hivyo Tanzania ingefungiwa mara moja.
TFF inasisitiza kuwa FIFA ilijua tatizo
la Serikali kutoa maagizo kwake kupitia vyombo vya habari, hivyo kumuandikia
Rais Tenga na kueleza msimamo wake iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa
ikiingilia uendeshaji wa shughuli za mpira wa miguu.
Uhalali wa kuwepo kwa barua ya FIFA
kwenda kwa Rais Tenga juu ya suala hilo
ulihojiwa pia na mwandishi wa Reuters, Brian Homewood baada ya kusoma kupitia
vyombo vya habari nchini kuwa Shirikisho hilo
huenda likaifungia Tanzania
ikibainika Serikali inaingilia shughuli za TFF. Mawasiliano kati ya FIFA na
mwandishi huyo ambapo majibu yake pia TFF ilipewa nakala yameambatanishwa
katika taarifa hii.
No comments:
Post a Comment