NA: BASHIR NKOROMO, DOGGUAN , CHINA
WATANZANIA wanaoshi nchini
hupo nchini China na ujumbe wa watu 14
kwa ajili ya ziara ya mafunzo katika nyanja mbalimbali, alikutana na Watanzania
hao, baada ya kuamua kumtembelea katika hoteli ya Exhibition International
hoteli, jana, Machi 12, 2013, ili kumsalimia na kubalishana naye mawazo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
Watanzania hao walisema, wamekuwa wakiishi nchini China kwa mahusiano
mazuri kutokana na maadili waliyolelewa nayo ya Kitanzania, lakini hali hiyo
huenda ikaingia dosari kutokana na kuwepo Watanzania ‘feki’ ambao wamekuwa
wakiingia China kwa pasi za Tanzania na kufanya maovu.
“Hawa Watanazania bandia wakiishaingia
hapa hujitambulisha kuwa ni Watanzania, hata wakiulizwa pasipoti ya Tanzania wanayo, lakini cha ajabu ukiwauliza
wanakotoka Tanzania
wanababaika na hata lugha ya Kiswahili hawajui sawasawa. Utamkuta mtu anajua
kusalimia tu, anasema ‘mambo’ basi, sasa jamani kuna Mtanzania ambaye hawezi
kuzungumza kiswahili, lakini akawa na uwezo wa kuja ugenini kama huku?” alisema
Katibu wa Jumuia wa Watanzania hao waishio China , David Chgamla.
Alisema, kutokana na hali hiyo, Wachina
sasa wameanza kupunguza imani yao
kwa Watanzania kiasi kwamba mtu anapojitambulisha kuwa ni mtanzania wakati
akiihitaji huduma anatazamwa mara mbili mbili kuthibitisha uaminifu wake.
Akizungumzia baadhi ya Watanyabiashara
kutapeliwa au kuziwa bidhaa zisizo na ubora au kwa bei isiyo halali, Katibu
huyo alisema, wengi wanakutana na mikasa hiyo kwa sababu wanakifika China wanakwenda mahali ambapo siyo sahihi kwa
mahitaji yao na
hivyo kutahamaki wakiingia hasara.
“Lakini Ndugu Kinana, Jumuia hii
tuliyounda hivi karibuni na kuwa na uongozi huu mpya, nina imani itawasaaidia
Watanzania wengi kutopoteza fedha au mali zao wanapokuwa wamekuja hapa
kibiashara, kwa sababu tunajipanga vema kuhakikisha kila atakayekuwa
anakuja akipenda anakutana na sisi kwa ajili ya msaada”, alisema.
Uongozi wa Wanajumuia hiyo ya Watanzania
unaundwa na John Luhumbiza (Mwenyekiti), Abraham Merishani (Makamu
Mwenyekiti), David Chamla (Katibu Mkuu) na Msaidizi wake ni Aboubakari
Mwinyi.
No comments:
Post a Comment