Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kulia) akizungumza na Naibu
Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa
Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming (kushoto)
baada ya kuwasili leo Machi 11, 2013 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Guangzhu, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku kumi nchini China. Katikati ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar )
Vuai Ali Vuai.
(Picha na Bashir Nkoromo).
NA BASHIR NKOROMO ,
CHINA
Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana amewasili leo Machi 11, 2013 nchini China kuanza ziara ya kikazi ya siku kumi, kwa
mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China .
Kinana ambaye ni
ziara yake ya kwanza kufanya nchi za nje tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa C
CCM, Oktoba mwaka jana, amewasili akiambatana na ujumbe wa watu 14 wakiwemo
viongozi na maofisa wa Chama na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa
Guangzhu, na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika
Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),
Wang Heming.
Katibu Mkuu ambaye aliwasili saa 8 mchana kwa saa za China (sawa
na saa nne asubuhi) za Tanzania, ameambataba na Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu wa
NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa Jumuia ya
Wazazi ya CCM, Khamis Suleiman Dadi, Katibu wa UWT Amina Makilangi, Katibu Mkuu
wa UVCCM, Martine Shigela na Wenyeviti wa CCM wa mikoa, Jesca Msambalavangu (Iringa),
Maganga Sengerema na Titus Kamani (Simiyu) na maofisa wa Chama.
Akizungumza
kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, Wang alisema, Chama Cha Kikomunisti cha
China kimefarijika na kuona fahari kubwa kwa kuupokea ugeni wa Kinana, kwa
sababu Katibu huyo wa CCM pamoja na kuwa ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa
kwake kuwa Katibu Mkuu wa CCM, pia ni kiongozi wa kwanza kutembelea China tangu
kupatikana kwa uongozi mpya wa China wa Rais Xi Jimping ambaye pia ndiye
Katibu Mkuu wa CPC.
Wang alisema,
kutokana na umuhimu wa ziara hiyo, uongozi wa juu wa CPC umeandaa ratiba
itakayomwezesha Kinana na ujumbe wake kushuhudia mambo mbalimbali ya
kimaendeleo katika nyanja mbalimbali za Uchumi na namna China chini ya
uongozi wa CPC ilivyofanya jitihada hadi kupiga mapinduzi makubwa ya kiuchumi
duniani.
Kwa Upande wake
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alishukuru kwa mapokezi makubwa
waliyotoa viongozi wa CPC, na kusema kueleza matumaini yake kwamba CCM
itakuwa na mengi ya kujifunza na viongozi hao kuondoka nayo kwa ajili ya kwenda
kuboresha na kuinua zaidi maendeleo ya Tanzania kiuchumi.
“Tunatambua ninyi
(China) mmekuwa washirika wetu wazuri na Tanzania tangu miaka mingi, kwa mfano
mmehusika sana katika ujenzi wa Reli ya TAZARA ambayo inatoa mchango mkubwa
katika uchumi wa taifa, na pia mmeshiriki kuanzisha viwanda nchini kwentu
kikiwemo kiwanda cha Urafiki pale Ubungo na bado mnaendelea kuwa washirikia
wazuri hadi sasa, kwa kweli tunafurahia sana ushirikiano huu”, alisema Kinana.
No comments:
Post a Comment