Tambalu aliyekuwa mwaka wa pili katika chuo hicho kilichopo
kwenye mji wa Wuhan , alifikwa na mauti hayo
Machi 17 mwaka huu wakati akiwa katika Uwanja wa Ndege mjini Beijing . Marehemu alikuwa Ofisa Kilimo
Mwandamizi kutoka wilayani Iramba mkoani Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Christina Midelo hakukubali wala
kukanusha kuwapo kwa tukio hilo .
“Sina taarifa za kifo cha kijana huyo, wanaoweza kuzungumza ni Ubalozi wa China kwa kuwa
ndio waliokuwa wakimsomesha.”
Balozi wa Tanzania
nchini China , Philip Marmo,
ambaye yupo nchini kutokana na ushiriki wake katika mapokezi ya Rais wa China , Xi Jinping, alikiri kufahamu suala hilo . Katibu wa Umoja wa
Wanafunzi wanaosoma vyuo mbalimbali katika mji wa Wuhan (Wtasa), Humphrey
Sikauki, alithibitisha kifo cha Tambalu na kwamba mwili wake ulikuwa unafanyiwa
uchunguzi na maofisa wa serikali ya China wakishirikiana na wale wa Tanzania.
“Tangu alipofariki madaktari walisema ripoti ingetolewa baada ya
siku saba ambazo ziliisha Jumatatu, mpaka sasa hiyo ripoti hatujaipata lakini
Mwambata wa Elimu katika Ubalozi wa Tanzania
nadhani atakuwa ameipata kwa sababu ndiye alikuwa akiiwakilisha Tanzania katika
uchunguzi huo,” alisema Sikauki.
Gazeti hili lilijaribu mara kadhaa kuwasiliana na Mwambata wa
Elimu katika Ubalozi wa Tanzania
nchini China ,
George Manongi lakini mawasiliano yalikuwa magumu, kutokana kushindwa
kusikilizana.
Kifo cha Tambalu
Tambulu ambaye alifika China Septemba 2011 kwa ajili ya masomo yake ya fani ya Kilimo, alifariki dunia akiwa katika Hospitali ya Chinese -Japanese Friendship.
Tambulu ambaye alifika China Septemba 2011 kwa ajili ya masomo yake ya fani ya Kilimo, alifariki dunia akiwa katika Hospitali ya Chinese -Japanese Friendship.
Habari zaidi zinaeleza kuwa, baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Beijing alianguka, kabla
ya kupelekwa hospitalini, ambako ilibainika kwamba alikuwa amekwishafariki.
Chanzo chetu kilidokeza kuwa, uongozi wa
hospitali ulitoa siku saba za uchunguzi kabla ya kutoa mwili wa marehemu,
lakini tatizo kubwa limekuwa ni uwezo wa kuusafirisha mwili huo.
Habari zinasema Wizara ya Kilimo haiwezi kuwajibika moja kwa moja kuusafirisha mwili wa marehemu isipokuwa halmashauri yake.
Habari zinasema Wizara ya Kilimo haiwezi kuwajibika moja kwa moja kuusafirisha mwili wa marehemu isipokuwa halmashauri yake.
Marmo kwa upande wake alisema ni vigumu
kwa Serikali kusafirisha mwili huo kwani haina bajeti ya masuala hayo na kwamba
yeye atachangia kama Watanzania wengine.
Habari zaidi zinasema Serikali yaChina imekataa kumsafirisha
marehemu kutokana na kifo hicho kutokuwa cha kawaida (natural death).
Habari zaidi zinasema Serikali ya
“Manongi aliwaambia ndugu wa marehemu Tanzania kuwa kampuni
aliyowasiliana nayo inaweza kusafirisha mwili huo kwa Dola za Marekani 40,000
au 45,000,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kinapasha pia kuwa, Mwambata huyo
aliwasiliana na mwajiri wa marehemu (Wizara ya Kilimo) kuhusu kumsafirisha na
mwajiri akakataa kwa sababu marehemu alikuwa mikononi mwa Serikali ya China .
“Alitaka ndugu wawajibike kuusafirisha mwili hadi nyumbani kwao
Shinyanga kwa mazishi,”kilisema.
Chanzo hicho kinaeleza kuwa, Mwambata pia aliwaeleza ndugu kuwa
chuo alichokuwa akisoma kilisema hakiwezi kuusafirisha mwili kutokana na ukubwa
wa gharama lakini kinaweza kuuchoma na kusafirisha majivu.
Gazeti hili liliwasiliana na Mwambata
huyo, lakini alipokuwa akipokea simu yake na mwandishi anamsikia lakini
kwa upande wake alikuwa hasikii hivyo kuitika tu “haloo, haloo…”
Alipotumia ujumbe mfupi wa maneno, alijibu kuwa simu yake imeshindwa kuutambua ujumbe huo kwani maandishi yalikuwa hayasomeki.
Alipotumia ujumbe mfupi wa maneno, alijibu kuwa simu yake imeshindwa kuutambua ujumbe huo kwani maandishi yalikuwa hayasomeki.
Chanzo: Mwananchi.
No comments:
Post a Comment