Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
ametaja wachezaji 23 watakaoingia kambini Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) jijini
Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco.
Mechi hiyo ya mchujo kuwania tiketi ya
kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil itachezwa Machi 24 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wa
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti
kambini katika hoteli ya Tansoma, Machi 17 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma
Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula (Azam),
Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris
(Azam), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani
(Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Nassoro Masoud Cholo (Simba) na Shomari Kapombe
(Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam),
Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo
(Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam),
Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa
(Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa
Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa
makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu),
Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Chanzo: TFF
No comments:
Post a Comment