Shughuli ya kuhesabu kura katika uchaguzi wa Kenya ingali
inaendelea kwa kujikokota, baada ya mashine za elektroniki kugoma na kisha
kutupiliwa mbali.
Makarani waliokuwa wanahesabu kura katika vituo vya kupigia
kura wamelazimika kupeleka karatasai zao katika kitovu cha kutangazia matokeo
ya kura ya urais katika ukumbi wa Bomas viungani mwa mji wa Nairobi .
Mgombea
wa urais Uhuru Kenyatta, ameweza kusalia mbele ya mpinzani wake Raila Odinga
kwa zaidi ya kura laki tano, lakini maafisa wa uchaguzi wanasema shughuli hiyo
huenda ikachukua muda.
Mkuu
wa tume ya uchaguzi ameonya kuwa huenda shughuli hiyo ikakamilika Ijumaa au
hata Jumatatu kabla ya mshindi kujulikana.
Wakati
huo huo Chama cha mgombea wa urais nchini Kenya , Uhuru Kenyatta, kimekosoa
uamzi wa tume ya uchaguzi , kwamba kura zilizoharibika zinapaswa kuongezwa
katika idadi ya kura zilizohesabiwa.
Hii
itapunguza kwa kiwango kikubwa uwezekano wa bwana Kenyatta , ambaye sasa
anaongoza kwa kura zilizohesabiwa.
Katiba
ya kenya inasena kuwa ili kufanya hivyo , kura zilizoharibiwa zinapaswa kuwa
zaidi ya nusu ya jumla ya kura zilizopigwa, lakini kwa sababu ya matatizo ya
mfumo wa kielektroniki , kura zilizoharibika tayari zimefikia zaidi ya laki
tatu .
Matatizo
ya kielektoniki yanaendelea , na maafisa wa Kenya wanasema matokeo rasmi huenda
yasitangazwe hadi mwishoni mwa juma.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment