Hii ni baada ya shahidi mkuu katika kesi hiyo kusema alitoa
ushahidi wa uongo.
Muthaura alihusishwa na ghasia za baada ya
uchaguzi Kenya
mwaka 2007 kwa kuwa mmoja wa wale waliopanga na kufadhili mashambulizi ya
uklipza kisasi dhidi ya jamii moja.
Kiongozi
wa mashtaka, Fatou Bensouda alisema anafutilia mbali mashtaka yote dhidi ya
Francis Muthaura ambaye anatuhumiwa kwa uhalifu ikiwemo mauaji na ubakaji baada
ya kutokea dosari katika ushahidi.
Wakati
huohuo mawakili wa rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta nao wanatarajia baadaye
leo kuwashawishi majaji katika mahakama hiyo kudurusu ushahidi ambao viongozi
wa mashtaka walitoa dhidi ya Kenyatta kwa tuhuma kuwa alihusika na ghasia za
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007
Mawakili
wa Kenyatta wanatarajiwa kutoa hoja yao
siku mbili baada ya Kenyatta kushinda uchaguzi wa urais , wa kwanza kufanyika
tangu ghasia za baada ya mwaka 2007.
Mawakili
wanasema majaji wanapaswa kudurusu kesi hiyo hasa baada ya shahidi mmoja kutoa
ushahidi wa uongo na hivyo kuhujumu kesi dhidi ya Uhuru na mshukiwa mwingine
Francis Muthaura.
Kenyatta
alishinda uchaguzi wa wiki jana licha ya kesi anayokabiliwa nayo katika
mahakama ya ICC kwa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji, ubakaji
na kuwalazimisha watu kuhama makwao.
Viongozi
wa mashtaka wanamtaja kama mmoja wa wahusika
katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Kenyatta,
ambaye ni mwanawe rais mwanzilishi wa Kenya , Jomo Kenyatta ni mmoja wa watu
matajiri wakubwa zaidi barani Afrika na anasisitiza kuwa hana hatia.
Kesi
dhidi ya Kenyatta itaanza mwezi Julai
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment