Zengwe kubwa katika mechi hiyo ya ligi kuu ya vodacom Tanzania bara kati ya Simba SC na Coastal Union, ni kuchelewa kufika wachezaji wa Simba, kuususia uwanja kwa kutopasha viungo kabla ya mechi na kukataa kupeana mikono na wachezaji wenzao wa Coastal Union kutoka Tanga.
Wagosi wa kaya hawakuwa na hiyana bali waliingia uwanjani na kuanza kupeana mikono na waamuzi badala ya wachezaji wenzao.
Akaanza kupewa mazoezi ya kudaka na mchezaji mwenzie ambae alikuja kitambo kidogo.
Kocha wa Simba Patrick Liewing kutoka Ufaransa alikuwa na kazi ya kuokota makopo, mh jamani uzee kazi...
Baadae kidooogo wakaanza kuingia wachezaji wa akiba wa Simba. Nyuma yao kikaja kikosi cha kwanza mpira ukaanza.
Mshambuliaji wa wagosi wa kaya Twaha Ibrahim 'Messi' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Simba Nassor 'Cholo' huku Abdi Banda beki wa Coastal Union akiwa tayari kutoa msaada. Dakika ya 45 Mrisho Ngassa aliifungia Simba bao la kwanza na baada ya dakika moja Haruna Chanongo akaongeza bao la pili katika dakika za nyongeza. Kipindi cha pili kilipoanza Coastal Union walikuja kwa kasi baada ya dakika nne tu Razak Khalfan akarudisha bao moja lakini mpaka kipyenga cha mwisho matokeo yakabaki hivyohivyo 2-1.
Malkia wa nyuki akiwa na furaha hapa anampa mkono Shomari Kapombe baada ya mechi kuisha 2-1. Malkia wa nyuki ndie mwenyekiti wa kamati ya ushindi Simba.
Jamani huyu kocha wa Simba ni mzee balaa, hapa ni baada ya mechi kuisha akizungumza na wanahabari, pembeni yake ni Boniface Wambura msemaji wa TFF.
wenyekiti wa klabu ya Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora'
Mkurugenzi wa ufundi wa Coastal Union na mmoja wa wadhamini wa timu Nassor Binslum.
Sifa moja wa wagosi wa kaya ni hizi ngoma, hata timu iende mbinguni hizi ngoma lazima waende nazo...
No comments:
Post a Comment