Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa
Katoliki, Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua
wafanyikazi wakuu watakaohudumu katika Vatican
chini ya uongozi wake. Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu
ya mtakatifu Maria Maggiore mjini Rome .
Baadaye
Papa atafanya misa ya sherehe katika kanisa la Sistine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya Papa
Francis, utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa
nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo .
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa
kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na
Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama
papa. Hata hivyo yeye mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya
Jumanne.
No comments:
Post a Comment