Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la mchezaji mkongwe wa Yanga
na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11,
2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye
alifariki jana usiku baada ya kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili,
atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha
stadi wa Pan Africa ambaye aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka
1982. Pia amefundisha nyota wengi wa kandanda nchini wakiwemo kina Kassim
Manara, Adolf Richard, Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao
walichezea Taifa Stars kutokea Yanga na Pan..
Baada ya kushiriki mazishi huyoooo akaanya safari mpaka Ikulu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Mzee`
Yusuf Mzimba, mmoja wa wazee marufu wa Klabu ya Dar es salaam Young Africans
(YANGA) ambaye amelezwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza
majeraha kufuatia kugongwa na BodaBoda wiki iliyopita Barabara ya Nyerere
jijini Dar es salaam.
Mzee Mzimba amevunjika mguu wa kushoto na kupata majeraha ya usoni
na mikononi. Hadi jana hali yake ilikuwa inaendelea vyema na Rais Kikwete
amempa pole nyingi kwa maumivu aliyoyapata na kumtaki apate nafuu ya haraka.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment