Moshi mweusi umetokea kwenye dari la hekalu ya Sistine
mjini Roma, kumaanisha kuwa makadinali walioko ndani ya hekalu wameshindwa
kuafikiana juu ya Papa mpya anayetarajiwa kuchaguliwa.
Moshi
mweupe utaashiria kupatikana kiongozi mpya wa kanisa Katoliki la Roma.
Makadinali
hao wanatarajiwa kupiga kura mara nne kwa siku hadi pale thuluthi mbili ya
makadinali wote watakapoafikiana juu ya Papa mpya.
Walipiga
kura yao ya
kwanza ambayo haikuleta maafikiano hapo usiku wa Jumanne. Yeyote atakayeteuliwa
kuliongoza kanisa hilo
katoliki anakabiliwa na wakati mgumu, ambapo kanisa limezongwa na kashfa mbali
mbali pamoja na migawanyiko ya ndani.
Papa
aliyeondoka Benedikt wa Kumi na sita aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu
wadhifa huo miaka minane tu tangu kuchaguliwa. Yeye ndiye Papa wa kwanza
kujiuzulu katika miaka 600 ya historia ya kanisa hilo .
Alitoa
sababu kuwa amezeeka na afya yake imedhoofika kwa hivyo haoni kuwa anaweza
kutekeleza wajibu wake kikamilifu kama Papa wa
kanisa.
No comments:
Post a Comment