.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), Absalom Kibanda amefanyiwa upasuaji wa kitaalamu bila kutumia kisu na
madaktari wanaomtibu katika Hospitali ya Milpark, Johannesburg , Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa TEF,
Neville Meena katika operesheni hiyo iliyofanyika juzi saa 5.30 asubuhi,
walipitisha mipira kwenye matundu ya pua na kutibu matatizo yaliyokuwa
yakimkabili ndani ya mwili wake.
Taarifa hiyo ilisema madaktari walichukua hatua hiyo ili kuepuka
kumwongezea majeraha zaidi mhariri huyo mtendaji wa New Habari (2006), ambaye
alikuwa na vidonda kutokana na kukatwakatwa na wavamizi.
Upasuaji aliofanyiwa ni pamoja na ule wa kuondoa jicho la
kushoto, pia kurekebisha taya lake la kushoto.
Taya hilo na meno ambavyo vilibainika kupata
mtikisiko vimefungwa waya maalumu ili kuvirejesha katika hali ya kawaida.
Kuhusu jicho lililong’olewa, madaktari wamepanga kumwekea jicho la bandia ambalo hata hivyo, halitamwezesha kuona.
Kuhusu jicho lililong’olewa, madaktari wamepanga kumwekea jicho la bandia ambalo hata hivyo, halitamwezesha kuona.
“Jicho hilo
linasubiri uamuzi wa madaktari wanaomtibu ambao wamesema wanasubiri kupona kwa
jeraha alilopata,” iliongeza taarifa hiyo.
Meena alisema katika taarifa hiyo kuwa Kibanda alikuwa na nafuu
kubwa jana kuliko ilivyokuwa siku za mwanzo.
Alisema madaktari walimweleza kuwa sura yake ilikuwa imeanza
kurejea katika hali ya kawaida na uvimbe wa damu umepungua.
“Tunamshukuru Mungu kwamba mwenyekiti wetu anaendelea vizuri
baada ya upasuaji wa saa 05.30 uliofanyika jana Jumamosi. Anazungumza vizuri
kiasi cha kuwatia matumaini wanaomuuguza,” alisema Meena katika taarifa hiyo na
kuongeza kuwa anaendelea kutumia dawa akiwa chini ya uangalizi wa madaktari na
wauguzi.
Milpark anakotibiwa Kibanda ni moja ya hospitali bora barani
Afrika ambayo hata Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela hutibiwa hapo.
Chanzo: Gazeti Mwananchi.
No comments:
Post a Comment