Christiano Ronaldo leo amekuwa mwiba kwa timu yake
ya zamani Man United baada ya kufunga goli moja katika mawili yaliyozamisha
jahazi la mashetani wekundu kuendelea na klabu Bingwa barani Ulaya.
Ronaldo alifunga goli la pili dakika ya 68 baada ya
Modric kusawazisha bao la kujifunga ndani ya dakika ya 48 lililowekwa kimiani
na mchezaji wa Madrid
Sergio Ramos.
Wapenzi wa soka duniani, leo macho yao yalikuwa kwa mchezaji
mkongwe wa Manchester United, Ryan Giggs aliecheza mechi yake ya 1,000 tangu
aanze kuichezea timu hiyo mwaka 1990.
Manchester United ya Uingereza leo ilikuwa na
kibarua kigumu dhidi ya Real Madrid ya Hispania, katika mchezo wa kihistoria wa
marudiano wa Klabu Bingwa Ulaya, uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford,
jijini Manchester .
Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika uwanja huo
ni miaka kumi iliyopita katika mchezo wa marudiano Klabu Bingwa Ulaya, ambapo Manchester United
ilishinda 4-3.
Hata hivyo, Manchester
United waliaga michuano hiyo kwa tofauti ya magoli 6-5, kwani katika mchezo wa
awali katika uwanja wa Bernabeu, jijini Madrid ,
Real Madrid
ilishinda 3-1.
Wakati Giggs na mashabiki wake wakisherehekea mechi
ya 1,000, mchezaji Cristiano Ronaldo kutoka Ureno wa Real Madrid amekuwa gumzo
la mashabiki hao kama ilivyokuwa kwa Ronaldo De Lima wakati timu hizo
zilipokutana kwa mara ya mwisho katika kombe kama hilo, April 23, 2003.
Aidha, Ronaldo De Lima kwa miaka hiyo, alikuwa akishutumiwa
kushuka kiwango kama ambavyo Cristiano anavyoshutumiwa kwa sasa, hasa wapinzani
wake wakipima kiwango chake na Lionel Messi wa Barcelona .
Hata hivyo, Ronaldo De Lima, alifunga midomo ya
mashabiki wa Uingereza kwa kutumbukiza mabao yote matatu, katika ushindi wa Manchester United wa mabao 4-3, mabao matatu hayo ya Real Madrid yote yakiwekwa
kimiani na Ronaldo.
Steve McManaman, kiungo wa Real Madrid wakati huo alisema: “Kila mmoja
alikuwa na hamu ya kumuona Ronaldo. Alituhumiwa sana kuhusiana na kiwango
chake, lakini kwa mabao matatu aliyofunga alidhihirisha alikuwa na uwezo mkubwa
katika mechi muhimu kama ile.”
Nadhani usiku wa leo historia ya Ronaldo wawili imejirudia kwani
mbali ya bao moja alilopata Crostiano lakini yapo mabao mengi zaidi ambayo
laiti yote yangeikia wavuni basi nae angetoka na magoli matatu kama mtangulizi wake Ronaldo De Lima.
HAFIDH KIDO
6 March, 2013
No comments:
Post a Comment