Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela amepelekea
hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.
Taarifa kutoka kwa afisa ya Rais wa Afrika Kusini zimesema
kuwa uchunguzi huu ni wa kawaida tu.
Kwa muujibu wa tovuti ya Urais wa Afrika
Kusini, Madaktari wanaomfanyia uchunguzi Mzee Mandela wamesema hakuna haja ya
kuwa na tahariku.
Kwa
muda mrefu sasa hali ya kiafya ya rais huyo mstaafu imekuwa ni swala la kutia
wasiwasi.
Mandela
mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini kwa siku 18 mwezi wa Desemba mwaka
jana kutokana na kutatizwa na mapafu pamoja vijiwe ndani ya kibofu chake cha
mikojo.
Taarifa
iliyoandikwa kwenye mtandao wa Ofisi ya Rais Jacob Zuma zimeeleza kuwa Mzee
Mandela alipelekwa katika Hospitali ya Mjini Pretoria kwa uchunguzi wa kawaida
wa ki-afya
Taarifa
hiyo imeendelea kusima kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutikana na matatizo
yanayoambatana na Umri wake mpevu.
Mzee
Mandela alifudumu kama rais wa Afrika Kusini
kati ya mwaka 1994 to 1999 na ndiye rais wa kwanza mweusi kuwahi kuitawala nchi
hiyo.
Kutokana
na juhudi zake za kupigania demokraisa na kupambana na sera za ubaguzi wa rangi
nchini humo, Mzee Mandela anatambulika kama
Baba wa Taifa nchini Afrika Kusini.
Tangu
mwaka 2004 Mzee Nelson Mandela amekuwa hajitokeza hadharani au kushiriki katika
shughuli za umma.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment