Wednesday, March 13, 2013

Game ya jana ilidhihirisha uwezo wa Barcelona si kazi ndogo kuifunga AC Milan mabao 4-0...

 David Villa akiweka kimiani bao la tau huku mchezaji wa AC Milan akiwa hana la kufanya kuokoa jahazi.

 Linel Messi akipachika bao la pili mbili ya wachezaji wawili wa AC Milan, ama hakika Milan jana walivurugwa.

 Halafu uniambie ati Messi kiwango chake kimeshuka, utakuwa hufuatilii soka la kimataifa wewe.

Ukimuona kama mpofu vile lakini wee chokoza uone moto. Huyo ndie mtoto Lionel Messi kutoka Argentina.

Messi alipachika mabao mawili peke yake katika dakika ya 5 na 39 kipindi cha kwanza na kufanya suluhu ya 2-2 kwani Barcelona waliingia uwanjani Camp Nou wakiwa nyuma ya mabao mawili mechi iliyopita.

kipindi cha pili kilipoanza David Villa aliwapa furaha mashabiki wa Barcelona kwa kuihakikishia timu yake kusonga mbele kwa kufunga bao la 3 dakikaya 57 na Jordi Alba ndie aliegongolea msumari wa mwisho wa jeneza la AC Milan kwa upacha bao la nne daa ya 90.

No comments:

Post a Comment