Makadinali wa kanisa katoliki la Roma wameanza shughuli ya
kumchagua papa mpya. Misa maalum imeandaliwa katika makao makuu ya kanisa hilo
Vatican, St. Peter's Basilica. Baada ya misa makadinali wote walio na umri wa
zaidi ya miaka 80 wataingia hekalu ya Sistine ambako upigaji kura utafanyika.
Makadinali
hao 115 watafungiwa ndani ya hekalu, bila mawasiliano na yeyote nje na
wataapishwa kuweka siri ya matukio yote wakati wa uchaguzi huo. Inaaminiwa kuwa
shughuli hiyo huenda ikadumu siku kadhaa.
Mwandishi
wa BBC mjini Roma anasema kuwa hakuna mgombea wa wazi anayetazamiwa kuchukua
mahala pa Papa mtakatifu Benedikt wa kumi na sita. Papa huyo aliwashangaza
wengi alipotangaza kujiuzulu baada ya kuhudumu miaka minane. Yeye ndiye papa wa
kwanza kujiuzulu katika miaka 600 iliyopita.
Maelfu
ya waumini wa madhehebu ya katoliki wamekusanyika nje ya kanisa la St. Peter's
Basilica, kufuatilia kwa karibu shughuli hii muhimu ya kumteua kiongozi mpya wa
kanisa. Makadinali waliochaguliwa watapiga kura mara nne kwa siku hadi pale
Papa mpya atakapo patikana. Kwingineko maelfu ya waumini wanatizama kwenye
televisheni na kusikiliza kwenye redio matukio ya Roma kujua iwapo wamepata
Papa.
Makadinali wafanya misa maalum
No comments:
Post a Comment