Kadinali
Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara
tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali
moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa
la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa
walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya
hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao .
Kadinali
Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi
uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali
115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao
kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa
inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza
kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na
kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani
angelichaguliwa.
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali
duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya
Jumanne.
Muda
mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana
wakikimbia kuelekea ukumbi wa St
Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .
Papa
Francis I ni nani?
Alizaliwa
Mjini Buenos Aires huko Argentina
mwaka1936.
Papa
Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu
kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.
Papa
Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari
Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina
miaka ya zamani.
Kama
kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali
Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina .
Hata
hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na
wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na
hasa watu maskini.
adinali
Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama
Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina .
Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari
mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005
Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi
wanasema utamsaidia sana
katika uongozi wake.
Katika
maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa
Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu
anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika
Kusini.
Bergoglio
anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado
linashikilia itikadi za kale.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment