Monday, March 4, 2013

UCHAGUZI WA KENYA KWA UFUPI:

 Wapiga kura milioni 14 wanategemewa kutenda haki hiyo leo, kuchagua viongozi sita: Rais, Gavana, Seneta, Mbunge, Mwakilishi wa wanawake na mwakilishi wa kaunti. Wagombea wanane wa Urais ni James Ole Kiyiapi, Mohammed Dida, Martha Karua, Musalia Mudavadi, Paul Muite, Raila Odinga, Peter Keneth na Uhuru Kenyatta.

Maafisa wachunguzi wa kimataifa ni 7,000, Maafisa wa polisi wanaolinda uchaguzi huo ni 99,000, wakati vituo 33,000 vimetengwa kwa kupigia kura. Mungu ibariki Kenya, Mungu ibariki Afrika. Uchaguzi uwe wa amani na utulivu.

No comments:

Post a Comment