Mabao matatu ya nyota wa TP Mazembe ya
DR Congo, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu yalitosha kuipa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ushindi mnono wa mabao
3-1 dhidi ya Morocco katika
mechi ya kutafuta tik-eti ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia , Brazil
2014.
Kwa ushindi huo, Stars sasa imefikisha
pointi sita na hivyo kuendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C ikiwa
nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, baada ya kuifunga Gambia mabao
3-0 juzi.
Mshambuliaji Ulimwengu aliyeingia
akitokea benchi kipindi cha pili alifunga bao la kwanza la Stars dakika ya 46,
kabla ya kumtengenezea nyota mwenzake wa TP Mazembe, Samata aliyefunga men-gine
mawili dakika ya 66 na 80.
Stars ilianza mchezo huo kwa kasi na
kulifikia lango la wapinzani wao dakika ya pili tu ya mchezo wakati shuti la
kiungo Amri Kiemba ilipogonga mtambaa wa panya kabla ya mabeki wa Morocco
kuon-doa mpira kwenye hatari.
Dakika ya tisa Morocco ilijibu
mapi-go na kona iliyochongwa na Barrada Abdellaziz ilimfikia Abuurazouk Hamza
ambaye alipiga kichwa kilichotoka senti-mita chache kwenye lango la Stars.
Baada ya kashikashi hizo, kila upande
ulijaribu kutuliza mpira chini na kupelekeana mashambulizi kwa zamu. Hata hivyo
hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika hakuna timu ili-yokuwa
imetingisha nyavu.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars
kuz-induka upya na kupeleka mashambulizi kuelekea kwa wapinzani wao Morocco na
kupata bao dakika moja tu kupitia kwa Ulimwengu, ambaye ulikuwa ni mpira wake
wa kwanza kuugusa.
Ulimwengu aliyeingia uwanjani kipindi
cha pili akichukua nafasi ya Mwinyi Kazi-moto alipachika bao hilo
kwa shuti kali la karibu lililomshinda kipa wa Morocco , Lamyaghir Nadir kutokana
makosa ya mabeki wake waliochelewa kuondosha mpira kwenye eneo lao la hatari.
Samata ambaye takriban muda wote wa
mchezo alikuwa kero kwa mabeki wa Morocco
alifunga bao lake la kwanza kwa shuti la pembeni baada ya kuwa-toka mabeki wa Morocco kisha
kufunga lingine kwa kumalizia pande la kukata la Ulimwengu.
Dakika ya 81, mwamuzi wa mchezo huo
Helder Martins kutoka Angola
alim-wonyesha kadi nyekundu Achachakir Abdelkarim wa Morocco baada ya kum-tolea lugha
chafu na kumsukuma aki-dai alitendewa faulo na Ulimwengu kabla hajatoa pasi ya
bao kwa Samata.
Katika mechi hiyo, kocha wa Taifa Stars,
Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 64, kwa kumtoa Ngasa nanafasi yake
kuchukuliwa na Athumani Iddi, pia dakika ya 89 alimtoa Samata na kum-wingiza
John Bocco.
Dakika ya 90, Chaeni Kamal alifunga bao la kufuatia machozi kwa
upande wa Morocco
na hivyo kufanya matokeo kuwa 3-1. Akizungumza baada ya mechi kumal-izika,
kocha Kim alisema: “Nimefurahish-wa na ushindi huu, vijana wangu waliji-tuma na
wanastahili ushindi, ninaomba Watanzania waendelee kuiunga mkono Taifa Stars.”
Alisema:
“Kipindi cha kwanza Moroc-co walikuwa wakijilinda na kufanya mashambulizi ya
kushtukiza huku wakitegemea pia mipira iliyokufa.”
Chanzo:
Mwananchi.
No comments:
Post a Comment