Wednesday, March 27, 2013

Dereva aliemgonga Traffic Bamaga huyu hapa...Dereva Jackson Simbo (43), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, kujibu shtaka la kusababisha kifo cha askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Elikiza  Nnko.
Mshtakiwa huyo, alifikishwa mahakamani jana.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ladislous  Komanya, alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Machi 18 mwaka huu, katika  eneo la Bamaga, Barabara ya Bagamoyo.
Wakili Komanya alidai kuwa  pamoja na shtaka  hilo, mshtakiwa  pia anakabiliwa na shtaka la kuingilia msafara wa kiongozi, kinyume na sheria. Wakili alidai kuwa akiwa katika sehemu hiyo ya  Bamaga, mshtakiwa  aliingilia msafara wa kiongozi na kushindwa kuheshimu maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara na askari huyo.
Komanya  aliendelea kudai,  Simbo pia anakabiliwa na  shtaka la  shindwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi hadi alipo tafutwa na vyombo vya dola.
Hata Hivyo kwa upande wake, mshtakiwa alikana tuhuma dhidi yake na Hakimu  Kwey  Lusemwa aliahirisha kesi hiyo hadi  Aprili 15, mwaka huu.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya wakili wake Edward  Chuwa, kuomba  mteja wake adhaminiwe kwa kuwa  ametimiza masharti ya dhamana.
Chanzo: Gazeti Mwananchi.

No comments:

Post a Comment