Jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga amesema kuwa
mahakama ya juu zaidi itasikiliza na kuamua bila mapendelo kesi iliyowasilishwa
katika mahakama ya juu zaidi kuhusu utata wa kura za urais.
Kesi hii imewasilishwa na muungano wa Raila odinga wa CORD
wakipinga ushindi wa Uhuru Kenyatta.
Bwana Mutunga aliyepokea stakabadhi zenye
matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais kutoka kwa tume ya uchaguzi Kenya , pia alisema majaji wa
mahakama hiyo ndio watasikiliza kesi hiyo.
Alisema
kuwa uchaguzi ulikuwa wenye amani na pia aliwashukuru wakenya kwa kuwa na imani
na idara ya mahakama.
Jaji
Mutunga alivitaka vyombo vya habari kupeperusha moja kwa moja kesi hiyo wakati
itakapokuwa ikisikilizwa ka sababu ya kuhakikisha uwazi.
Mgombea
wa urais aliyeshindwa, Raila Odinga , Jumapili aliunda kikosi cha mawakili
watakaowasilisha kesi dhidi ya ushindi wa Uhuru Kenyatta kama rais wa nne wa
Jamuhuri ya Kenya, kama alivyotangazwa na tume ya uchaguzi na mipaka Kenya.
Odinga
anataka mahakama iamuru kuhesabiwa tena kwa kura na kuchunguza visa vya
kupungua maradufu kwa kura za urais kutoka maeneo bunge fulani baada ya sajili
la wapiga kura kufungwa.
Pia
wanahoji uwezekano wa wapiga kura milioni moja kumpigia kura rais peke yake
bila kumchangua mtu mwingine akisema kuwa huenda wakawasilisha kesi hiyo
Jumatano.
Kenyatta
alimshinda Odinga kwa kura laki nane na kupata zaidi ya asilimia hamsini na
moja ya kura zilizopigwa.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment