Sunday, March 17, 2013

Makamu wa Rais Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal afanya ziara Ruvu kuangalia maji.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi Mji mpya wa Mabwe Pande (hawapo pichani) wakati alipofika katika mji huo jana Machi 14, 2013 akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Maji inayosimamiwa na Dawasa na kutembelea katika Mtambo wa Ruvu Chini kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kulia ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidik. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa Dawasa baada ya Makamu kutembelea na kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Ruvu chini, jana Machi 14, 2013. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment