Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini(trafiki), Mohammed
Mpinga alisema hayo jana alipozungumzia tukio hilo ambalo lilisababisha simanzi
kwa watu wengi.
Mpinga alisema polisi walifanikiwa kumkamata mhusika kwa mbinu
za kipolisi na kwamba kwa jana alikuwa akihojiwa ili kupata ushahidi
utakaowezesha kumpeleka kortini.
Alisema dereva huyo ni kati ya wale wawili
waliowakamata awali na hatimaye mmoja walimbaini kuwa ni
mhusika .
‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao alitudanganya,
tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo mimi nimeachiwa na
mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na kuongeza kuwa baada ya kumbana
alikiri kuwa ndiye.
Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga marehemu ameacha mume na watoto
watatu. Maziko yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Mbweni yaliyopo
Manispaa ya Kinondoni na yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Marehemu alifariki dunia baada ya kugongwa na gari
lililokurupuka kuufuata msafara wa Rais Jakaya Kikwete eneo la Bamaga Mwenge
jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita alipokuwa katika ziara ya kutembelea
mkoa huo.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment