Wednesday, March 13, 2013

DRFA yateua kamati ya utendaji kujiimarisha...


DAR ES SALAAM REGION FOOTBALL ASSOCIATION (DRFA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
12th MARCH 2013

Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kwa mamlaka iliyonayo imeteua kamati mbali mbali zitakazoshirikiana na Kamati ya Utendaji katika kukabiliana na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu katika Mkoa wake ili kuweza kufikia malengo yake waliyojiwekea. Wafuatao ni watu na kamati mbali mbali walioteuliwa/zilizoteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam:

Bw. Joseph Kanakamfumo                     Mkurugenzi wa Ufundi
Bw. Saidi Pambalelo                              Afisa Tawala
Bw. Mohamedi Muharizo                       Afisa Habari
Bw. Hashim Abdallah                             Afisa Usalama

KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO
1.       Bw. Meba Ramadhani               Mwenyekiti
2.       Bw. Iddi Msonga                       Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Ali Hassani                                                  
4.       Bw. Ramadhani Kilemile
5.       Bw. Isack Mazwile

KAMATI YA UFUNDI NA MASHINDANO
1.       Bw. Kenny Mwaisabula              Mwenyekiti
2.       Bw. Shabani Mohamedi              Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Hugo Seseme
4.       Bw. Daudi Kanuti
5.       Bw. Kassim Mustapha
6.       Bw. Abeid Mziba
7.       Bw. Bakari Mtumwa

KAMATI YA MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA NA WANAWAKE
1.       Bw. Benny Kisaka                     Mwenyekiti
2.       Bw. Muhsin Balhabou                Makamu Mwenyekiti
3.       Dr. Sesy Makafu
4.       Bw. Emmanuel Kazimoto
5.       Dr.  Maneno Tamba
6.       Bw. Edwin Mloka
7.       Bw. Sande Mwanahewa
8.       Bw. Richard Shayo

KAMATI YA WAAMUZI
1.       Bw. Jovin Ndimbo                     Mwenyekiti
2.       Bw. Sijali Mzeru                        Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Saidi Mbwana
4.       Bw. Benny Mtula
5.       Bw. Abdallah Mitole

KAMATI YA NIDHAMU NA USULUHISHI
1.       Mheshimiwa Roman Masumbuko            Mwenyekiti
2.       Bw. Fahadi Faraji Kayuga                       Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Mohamedi Mpili
4.       Bw. Peter Nkwera
5.       Bw. Jimmy Mhango

KAMATI YA RUFAA
1.       Mheshimiwa Salehe Njaa                       Mwenyekiti
2.       Bw. Saidi Engo                                      Makamu Mwenyekiti
3.       Bw. Abasi Kuka
4.       Bw. Yusuph Macho
5.       Bw. Boi Risasi

Pia Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam inapenda kuwafahamisha wanachama wake, wadau na mashabiki wa mpira wa miguu Tanzania dhamira yao ya kuendeleza mpira wa miguu katika Mkoa wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Kwa kuanzia Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kipo kwenye mchakato wa kukamilisha DRFA Strategic Plan 2013 - 2016 (Mpango Mkakati Kazi) kwa kipindi cha miaka minne pamoja na kuboresha Financial Regulations zake ili kiweze kuwa na dira ya kuwahudumia wadau wake kwa ufanisi na uwazi zaidi. Lakini pia Kamati ya Utendaji imeona haja ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na Website yake kwa ajili ya kuwapa habari wadau wake na Watanzania kwa ujumla.

Mwisho Kamati ya Utendaji ya Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam kinaomba ushirikiano na wadau wote wa mpira hususani Serikali, TFF, Vyama vya Mikoa, Walimu, Waamuzi, Madaktari, Vilabu, Makampuni na Waandishi wa habari na Vyombo vya habari katika kuendeleza mpira wa miguu katika mkoa wa Dar es Salaam na hatimaye mikoa yote ya Tanzania. “Kwani Pamoja Tunaweza”

Ahsanteni,

Almasi Kasongo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)

No comments:

Post a Comment