Wednesday, March 6, 2013

Kuvamiwa kwa wanahabari na wanaharakati Tanzania...

Inashangaza sana leo asubuhi dunia ya wanahabari Tanzania ilisimama kwa muda baada ya mwanahabari nguli mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na mhariri mkuu wa New Habari Ambsalom Kibanda kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa jana akiwa nyumbani kwake saa sita usiku wakati akirejea kutoka kazini.

Kibanda amekatwa kidole, ametolewa meno, kutobolewa jicho moja na kukatwa mapanga kichwani. Kwa sasa yupo hoi Hospitali ya Taifa Muhimbili akipambana na maisha yake. Tanzania imepatwa na nini?


Kesho asubuhi habari hii tutaipata kwa kina baada ya taarifa sahihi kutoka kwa watu wa karibu wa Kibanda kuzunumza na wanahabari.

Ila mpaka sasa Hussein Bashe ambae ndie afisa mkuu wa kampuni ya New Habari, anahangaika na mdhamini wa Kibanda pamoja na wanasheria wake ili kupata pasi ya kusafiria ya Kibanda ili aweze kupelekwa nje kwa matibabu zaidi maana leo asubuhi ndiyo siku ambayo alitakiwa kuripoti mahakaman kwani ana kesi mahakamani aliyoipata wakati akiwa mhariri mkuu gazeti la Tanzania Daima mwaka jana.

Serikali ilizuia pasi yake ya kusafiria hivyo ili aweze kupelekwa nje lazima iombwe.....

HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
6 March, 2013
Dar es Salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment