Tuesday, March 5, 2013

Serikali ya Venezuela imetangaza kuwa tatizo la kushindwa kupumua la rais Hugo Chavez limekuwa baya zaidi, na anaumwa maambukizi makali ya pumu.Katika taarifa iliyotolewa kwenye Televisheni ya taifa waziri wa habari , Ernesto Villegas amesema kuwa rais yuko mahututi.
Serikali bado haijatoa maelezo zaidi ya hali ya afya ya Bwana Chavez, tangu alipokwenda Cuba kwa matibabu ya saratani mapema mwezi Disemba.
Alirejea , lakini waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment