Waandishi Wetu,
Baada ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda kutekwa na watu wasiofahamika na kisha kumjeruhi vibaya kwa nondo, mapanga na kisha kumng’oa meno, kucha na kumharibu jicho la kushoto jana amesafirishwa kuelekea Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Baada ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda kutekwa na watu wasiofahamika na kisha kumjeruhi vibaya kwa nondo, mapanga na kisha kumng’oa meno, kucha na kumharibu jicho la kushoto jana amesafirishwa kuelekea Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Mbali ya mke wa Kibanda mtu mwengine alieandamana nae katika safari hiyo ni daktari kutoka taasisi ya mifupa hosiptali ya Muhimbili (MOI).
Tukio la kuvamiwa mwandishi huyo nguli linafanana kwa kiasi fulani na lile la alilofanyiwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari
Tukio
Mkasa wenyewe
Akizungumza kwa tabu alipokuwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi
maalumu (ICU), hospitalini Moi, Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New
Habari (2006), alisema:
“Nilifika nyumbani kwangu
“Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na kuanguka wakanifuata...niliona
“Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga
Mashuhuda baada ya tukio
Akizungumza jana, mzazi mwenzake, Angella Semaya alisema wakati Kibanda alipovamiwa hakusikia lolote: “Niliamshwa na kelele za majirani ndipo nami nikaenda eneo la tukio. Sikuamini kama alikuwa Kibanda kwani alikuwa ametapakaa damu huku akigugumia maumivu makali... kwanza sikumjua
“Nina wasiwasi na hawa watu kuwa wametumwa kwa kuwa hawakuchukua chochote zaidi ya kumdhuru mwili,” alisema. Angella aliondoka jana na Kibanda pamoja na Mwandishi wa Habari, Eric Kabendera ili kumsindikiza Afrika Kusini atakapokuwa anapata matibabu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Hussein Bashe alisema: “Tulikuwa na Kibanda hadi usiku kama 5:30 hivi, tukifuatilia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa
“Kwa kweli taarifa za kuvamiwa na kushambuliwa kwake zimetushtua, kwani ameumizwa
“Nawashukuru madaktari kwa jinsi walivyompokea na kumshughulikia katika kiwango kinachotia moyo. Pia waandishi kwa umoja waliouonyesha kwa kujitokeza haraka na kumjulia hali.”
Tasnia ya habari
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limeelezea kushtushwa na tukio la kutekwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa mwenyekiti wake.
Taarifa ya TEF iliyotolewa jana na Katibu wake, Neville Meena, imesema shambulio
Alisema mwendelezo wa vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari ambavyo katika siku za karibuni vimeibuka, vinalifanya jukwaa liamini kwamba wanahabari sasa wanatishwa ili wasiweze kutekeleza majukumu
“Utesaji huu aliofanyiwa Kibanda unafanana na ule aliofanyiwa Dk Ulimboka. (Rejea vitendo vya kupigwa kichwani, kung’olewa kucha na meno).
Aidha, Meena alisema: “Tunaamini kwamba yaliyomkuta Kibanda hayawezi kutenganishwa na msimamo wake kikazi au
"Tunaamini vyombo vya dola, vitachunguza na kuwatia mbaroni kisha kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa tukio hili na mengine kadhaa ambayo sasa yamegeuka kuwa sehemu ya utamaduni katika nchi yetu.”
Awali, Mjumbe wa Bodi ya TEF, Theophil Makunga alisema wakati huu wanahabari na wanafamilia wakisubiri uchunguzi juu ya tukio
“Hatuwezi kusema nini chanzo cha tukio
Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Jesse Kwayu alisema tukio
Mhariri wa Habari wa Tanzania Daima, Edson Kamukara alisema: “Matukio ya kutekwa na kushambuliwa kwa waandishi wa habari yamekuwa yakishika kasi... ni jambo la kusikitisha na hatuwezi kukaa kimya kwa hili.”
Baada ya tukio
Katika taarifa yake jana, Dk Nchimbi alisema Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ameteua timu ya maofisa wa polisi wanne kutoka Makao Makuu ya Upelelezi kuungana na wapelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Polisi Mkoa wa Kinondoni ili kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.
Baadaye jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema ofisi yake imeunda jopo la maofisa wa polisi tisa ambao wameshaanza kazi ya upelelezi wa tukio
Kova alisema kitendo alichofanyiwa Kibanda si cha kihalifu, bali kukomoana na visasi kwa kuwa upelelezi wa awali umeonyesha kuwa waliomvamia hawakuchukua chochote.
Akizungumzia tukio hilo ,
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene alisema Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia idara yake imepokea kwa mshtuko
tukio la kupigwa na kutendewa ukatili.
Alisema kitendo kilichofanywa kwa mhariri huyo ni ukatili uliopitiliza na kwamba wanaliachia Jeshi la Polisi lifanye kazi yake.
Wamjulia hali
Kabla ya Kibanda kupelekwa Afrika Kusini, viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal walifika kumjulia hali. Wengine ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene na Yussuf Omar Chunda na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk Reginald Mengi.
Mengi na Mbowe Akizungumza tukio
Alisema kuna haja ya polisi kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli halisi upatikane na wahusika wafikishwe katika vyombo vya sheria.
Mbowe alisema: “Tuungane katika kutetea uhuru wa vyombo vya habari. Uvamizi wa Kibanda ni doa kubwa katika tasnia ya habari bila kujali yuko chombo gani na yeye ndiye mkuu wa Jukwaa la Wahariri, ni wazi atakuwa amezungukwa na maadui wengi.”
Imeandikwa na Joyce Mmasi, Aidan Mhando, Bakari Kiango, Salhim Shao, Beatrice Moses na Aziza Masoud.
Chanzo: gazeti Mwananchi.
�
No comments:
Post a Comment