27 Machi, 2013 -
Saa 14:08 GMT
·
Mahakama hiyo imefutilia mbali uamuzi wa rais
Mosri kumteua mwendesha mkuu wa mashtaka mwingine Talat Ibrahim.
Hatua ya Bwana Morsi kumfuta kazi Abdel Maguid
Mahmoud, iliwaudhi sana majaji wakuu walioina
kama hatua ya kuhujumu mamlaka yao .
Hii ilikuwa hatua ya kwanza kama
hii kutokea baada ya rais Mosri kujiongeza mamlaka makubwa.
Hatua ya rais Morsi iliindolea idara ya
mahakama mamlaka yake ya kuweza kubatilisha uamuzi wowote tatanishi alioutoa .
Lakini rais Morsi baadaye alibatilisha uamuzi wake baada ya maandamano makubwa
kumpinga.
Kiongozi wa mashtaka wa sasa bwana Mahmoud,
aliteuliwa na rais wa zamani Hosni Mubarak.
Aidha Talaat Ibrahim naye alitakiwa kudurusu
uchunguzi kuhusu vifo vya waandamanaji waliopinga serikali ya Mubarak.
Afisaa mkuu wa serikali aliambia BBC kuwa
serikali itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini Misri.
Bwana Morsi amekabiliwa na matatizo chungu
nzima tangu kuchukua mamlaka mwezi Juni mwaka 2012 baada ya uchaguzi wa kwanza
kufanyika tangu kuondolewa mamlakani kwa Mubarak.
No comments:
Post a Comment