Serikali za Sudan
na Sudan kusini zimesaini
mkataba mpya wa kurejelea uchimbaji na usafirishaji wa mafuta kutoka Sudan Kusini kupitia mabomba ya Khartoum .
Mkataba
huu unakomesha mzozo uliokuwa kati ya nchi hizo mbili kwa muda wa mwaka mzima.
Serikali ya Juba ilikatiza uchimbaji mafuta
Januari mwaka uliopita kufutia mtafaruku juu ya ada zinazotozwa.
Waziri
wa habari wa Sudan
ya kusini Barnaba Marila Benjamin, ameambia BBC kuwa nchi hizo zimeafikiana na
kusaini mkataba juu ya ugawaji wa fedha za mafuta kufuatia upatanishi
ulioongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Nchi
hizo mbili zilitishia kuingia vitani kutokana na mvutano hasa juu ya mafuta na
mipaka tangu Sudan
ya Kusini ijitenge kuwa huru mwaka wa 2011.
No comments:
Post a Comment