Mwili wa hayati Hugo Chavez utakaushwa na kuwekwa katika
makavazi ya kijeshi nchini Venezueal. Mwili wa Chavez hautazikwa kwa siku
nyingine saba ili kuwaopa wananchi fursa ya kuuuona kabla ya kuzikwa.
Serikali ya Venezuela
imetangaza siku saba zaidi za maombolezi kabla ya kufanyika maziko ya marehemu
rais wa nchi Hito Hugo Chavez baadaye leo.
Serikali hiyo imeongeza muda wa maombolezi
kufuatia kufurika zaidi watu wanaotaka kutoa heshima zao za mwisho kwa
marehemu.
Makamu
wa rais , Nicolas Maduro, amesema kuwa mwili wa bwana Chavez utakaushwa na
baadae kuwekwa ndani ya kaburi la vioo ambapo utakuwa ukionekana.
Amesema
kuwa serikali imeamua kuchelewesha uamuzi wa mazishi yake kwasababu zaidi ya
raia milioni mbili wamekuwa wakipanga mstari kwa saa nyingi kwa ajili ya
kupokea jeneza la chavez linalopita.
Maafisa
wanasema kuwa bwana Maduro ataapiishwa kama
rais wa mpito baadaye leo na uchaguzi kufanyika baadaye.
Hugo
Chavez, aliyeongoza Venezuela
kwa miaka 14, alifariki baada ya kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Zaidi
ya viongozi 30 kutoka nchi mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Chavez
baadaye leo akiwemo rais wa Iran ,Mahmoud
Ahmadinejad, rais wa Cuba Raul Castro na rais wa Belarus Alexander Lukashenko.
Rais
Ahmadinejad amemsifu Chavez kama mpigania haki na kiongozi mwenye kuleta
mageuzi.
Wabune
wawili wa bunge la Congress la Marekani watawakilisha nchi hiyo katika mazishi
haya ikikumbukwa kuwa Chavez alikuwa mkosoaji mkubwa wa Marekani.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment