Siku nne baada ya kupiga kura wakenya wangali kujua
mshindi, wa urais, baadhi ya yaliyojitokeza hadi sasa ni pamoja na malalamishi
ya muungano wa CORD wake Raila Odinga kutaka tume ya uchaguzi kusitisha
shughuli ya kuhesabu kura wakidai kufanyika udanganyifu.
Leo mashirika ya kijamii yamekwenda mahakamani kuitaka
mahakama kuu kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura
Nayo tume ya uchaguzi yasema idadi kubwa ya
kura zilizoharibika ilitokana na hitilafu katika mtambo wake ambao ulikuwa
unaongeza idadi ya kura hizo mara nane
Hadi
kufikia sasa Uhuru Kenyatta ana kura 5,004,406 Raila Odinga ana kura 4,442,923
Wakenya
wakiwa katika kipindi kigumu na cha wasiwasi kwani imechukua Tume ya Uchaguzi
muda wa siku nne tangu kuanza shughuli ya kuhesabu kura na bado mshindi
hajajulikana.
Kumekuwa
na kila aina ya matukio katika muda huo wote. Tayari mashirika ya kijamii
yameitaka mahakama kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura inayofanywa
na tume ya uchaguzi.Muungano wa CORD unaoongozwa na tume ya uchaguzi,
umelalamika ukisema shughuli hiyo ina mizengwe na wanataka ianzishwe upya.
Tupe
maoni yako kwenye ukurasa wetu wa BofyaFacebook kuhusu
yanayojiri Kenya
na tutauweka ujumbe wako kwenye mtandao wetu Bofyabbcswahili.com
15:40Dennis Tsunami Mbaka anasema kupitia Bofyafacebook mataraiio
ya wakenya ni mengi na licha ya kuzuka mambo mengi wakati huu wa uchaguzi
hususan matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa, anachotaka ni mchakato mzima
kukamilika bila tashwishi na anaitakia nchi yake mustakabali mwema
15:32 Kuhusu kesi ambayo
mashirika ya kijamii yameishtaki tume ya uchaguzi na kuitaka ikomeshe shughuli
inayoendelea ya kuhesabu kura za urais, ni mapema mno kwa hilo . Duru za kisheria zinasema kuwa kesi
hiyo ina misingi duni kwani wanapaswa kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi
kutangazwa ndiposa waende mahakamani
15:25 Mwenyekiti wa tume ya
uchaguzi Isaack Hassan anatarajiwa kuhutubia waandishi wa
habari wakati wowote kuanzia sasa
15:21Hanif Mohammed akiwa mjini Mombasa
ameandika kwenye ukurasa Bofyafacebook akizungumzia
matokeo ya uchaguzi kwa sasa ya wagombea wakuu kuwa wanakanganywa na hesabu ya
kura hizi ila anachoomba tu ni kuwepo amani
15:14 Sebastian Sabato kwenye ukurasa wa Bofyafacebook anasema,
ijapokuwa ninasubiri matokeo kwa hamu na gamu, kwa upande mwingine shughuli
zangu zinaendelea kama kawaida.
wakati huohuo imeripotiwa kuwa:
Mahakama ya juu nchini Kenya
hii leo itatoa uamuzi ikiwa ina uwezo wa kusikiliza kesi iliyowasilishwa kwake
na makundi ya kijamii yakitaka tume huru ya uchaguzi nchini Kenya kusitisha shughuli ya
kuhesabu kura za urais inayoendelea katika ukumbi wa Bomas.
Makundi hayo yanadai kuwa tume inakwenda kinyume na katiba
ambayo ambayo inasema kura zinapaswa kuhesabiwa kwa njia ya elektroniki.
Pia Muungano wa Cord wake mmoja wa wagombea wa
urais Raila Odinga umedai kuwa tume hiyo inafanya hujuma katika shughuli ya
kujumlisha kura za urais katika ukumbi wa Bomas.
Hapo
jana Muungano wa CORD ulielezea malalamishi kuhusu shughuli yakujumlisha kura
za urais na kusema hauna imani nayo kwani ina ushahidi kuwa hujuma imefanyika
wakidai wizi wa kura.
Pia
wanadai kuwa katika baadhi ya maeneo, kura zilizopigwa ni nyingi kuliko idadi
ya wapiga kura waliosajiliwa.
Madai
haya waliyatoa hapo jana ingawa mkuu wa tume ya uchaguzi aliyakanusha vikali na
kusema hakuna mahala popote ambapo wameshuhudia matokeo kuhujumiwa.
Chama
hicho pia kilidai kuwa baadhi ya matokeo yalikuwa juu ikilinganishwa na idfadi
ya wapiga kura.
Na
kwa hilo , mkuu wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan
pia alikanusha vikali akisema hawajapata matokeo kama
hayo.
Tume
hiyo imesisitiza kuwa shughuli ya kuyahakiki matokeo inafanywa mbele ya
maajenti wa vyama vyote.
Wakati huohuo tume hiyo imekiri kuwa kulikuwa
na tatizo la mtambo wake wa kupeperusha matangazo ikisema kuwa ilikuwa
inaongeza mara nane kura zilizoharibika.
Washika
dau wengi walieleza wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya kura zilizoonekana
kuharibika kwani zilikuwa kura zaidi ya laki tatu. Lakini kufikia sasa
zimepungua na kufika themanini.
Mkuu
wa tume hiyo, Issack Hassan alisema kuwa komputa ilikuwa inaongeza idadi ya
kura zilizoharibika kwa mara nane.
Shughuli
ya kukusanya matokeo ilianza upya kwa mikono kufuatia matatizo haya lakini
Uhuru Kenyatta angali anaongoza dhidi ya Raila Odinga.
"kulikuwa
na makosa kwa namna ambavyo programu ya komputa ilikuwa imeundwa, '' alisema
Hassan.
''Kwa
kura zote zilizoharibika kwa kila mgombea zilikuwa zinaongezeka mara nane ,''
aliongeza kusema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment