Aliugua
saratani kwa muda mrefu na kufanyiwa upasuaji nchini Cuba , jambo lililomfanya asionekane
hadharani kwa miezi kadhaa.
Rais
Obama , ambaye nchi yake imekuwa na uhusiano mgumu na rais Chavez amezungumzia
juu ya kipindi cha changamoto kinachoikabili Venezuela
na kuongeza kuwa Marekani itatoa msaada kwa watu wa Venezuela .
Balozi
wa Urusi katika umoja wa mataifa Vitaly Churkin amesema kuwa bwana Chavez
amekuwa mwanasiasa shupavu kwa nchi yake , kwa eneo la Amerika ya kusini na
dunia kwa ujumla.
Naye
rais wa Argentina
, Cristina Fernandes de Kirchner, amesema kuwa ameakhirisha shughuli zake zote
baada ya kusikia taarifa ya kifo cha rafiki na mshirika wake .
Rais
wa Cuba Fidel Castro amesema anaomboleza kifo cha mtu ambaye alikuwa kama kijana wake.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment