Monday, December 3, 2012

Jamani leo watanzania tulio Kampala tuende kuishangilia timu yetu Taifa Stars inacheza na Rwanda....

Jamani Mrisho Ngassa noma, amekuwa mfungaji mwenye magoli mengi kuliko yeyote katika michuona tena magoli hayo aliyapata katika mechi moja tu dhidi ya Somalia. tazama msimamo, mrisho Ngasa (Tanzania) 5, John Bocco (Tanzania) 4, Umony (Uganda) 3, Ndikumana (Burundi) 3, Nduwagira (Burundi) 3, Msowoya (Malawi0 3, Birori (Rwanda) 2, Ochieng (Kenya) 2, Mcha (Zanzibar) 2 na Miheso (Kenya) 2.

Leo tunacheza na Rwanda uwanja wa Lugogo saa nane kamili, halafu baadae saa kumi katika uwanja huohuo wa Lugogo Zanzibar Heroes wanacheza na Burundi. Jamani angalieni Super Sport kama mpo nje ya Kampala. Ila kama mpo kampala njooni tuishangilie timu yetu.... Leo nitajitahidi kupata Camera nipige picha walau nanyi mpate zawadi...

Hafidh Kido
Kampala, Uganda

No comments:

Post a Comment