SUNDAY, DECEMBER 2, 2012
Ufafanuzi kesi ya Dowans
Ufafanuzi kuhusu gharama za uendeshaji kesi ya Dowans. Juzi
kwenye harambee ya M4C nilisema kwamba kabla ya kwenda Mwanza nilikuwa nafanya
mahesabu ya kiwango cha gharama ambazo TANESCO imetumia na ina mwelekeo wa
kutumia kwenye kesi ya Dowans pekee nikasema ni dola zaidi ya milioni 29
(ambayo ni bilioni takribani zaidi ya 40).
Nitoe ufafanuzi kwamba katika mahesabu yangu nimejumuisha USD
2.9 ml/- (takribani bilioni 4) za gharama za mawakili katika mazingira yenye
utata. Na gharama za kibenki iliyowekwa Uingereza katika mazingira ya hatari ya
kupoteza (risk) ya dola zaidi ya milioni 28 (bilioni zaidi ya 40) na gharama
nyinginezo ambazo nitazikokotoa baadaye. Ni vizuri mkarejea hotuba niliyoitoa
bungeni tarehe 27 Julai, 2012 ambapo nilitaja namna kesi za Dowans, IPTL,
zinavyotumiwa kifisafi kama vitega uchumi kwa
gharama zenye kubebesha mzigo kwa Tanesco na hatimaye wananchi kupitia bei ya
juu ya umeme.
John Mnyika,
Waziri Kivuli, Wizara ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment