Wanasiasa wawili wa Kenya wanaotaraji kugombea uongozi na
ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo
baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa wanaungana katika uchaguzi mkuu wa
mwaka ujao.
Katika mkutano wa
hadhara uliofanywa mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema
atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea
mwenza wa Bwana Kenyatta.
Siku
ya Ijumaa shirika la Kenya
la kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha
kesi mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka.
Wanasiasa
wengine maarufu wa Kenya
piya wameshtakiwa na ICC.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment