Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache
zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia
virago Chama cha Baba yao
CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na
Katibu Mkuu wa Chadema Dr
Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira. Wakizungumza na waandishi wa
habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:Ester wasira: (Ni
mwanasheria, graduate wa UDSM) (i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi
wa dhati wa Mtanzania. (ii) Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania
hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata
kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila
matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk (iii) CCM imedumaza nchi, nchi
imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu
mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na
kukua tena. (iv) Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake
wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania
mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili
kuijenga Tanzania
mpya. Alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja.
Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO): (i) Alielezea furaha yake kwa
kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania (ii)
Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi
itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura
(iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya
kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu
ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama
mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM
imeshindwa kuongoza nchi (iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka
50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo
mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa
miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo. (v) Anasema ana imani na sera
za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe
na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo
tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama
itambidi afanye hivyo. (vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu
isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura. (vii) Nae
alimalizia kwa kusema “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.”Dr Slaa
alitiwa moyo sana
na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo
waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.
No comments:
Post a Comment