Wateja milioni 2.5 wa Simu za mikononi leo
wamekuwa mashakani baada ya Tume ya Mawasiliano nchini Kenya kuzima simu
zilizotengenezwa kwa viwango vya chini (maarufu za kichina).
Zoezi hilo la kuzima simu lilianza
kutekelezwa usiku wa manane na linalenga kukabiliana na uingizaji wa simu
bandia, suala linalohujumu juhudi za kuimarisha usalama.
Hatua ya kuzima simu hizo na ambayo
imethibitishwa na kampuni nne za huduma za simu nchini humo, inafuatia agizo la
tume ya wasiliano nchini humo ambayo inataka kukabiliana na biashara haramu,
wizi wa haki miliki na tisho la usalama.
Afisaa mkuu mtendaji wa tume hiyo, Francis
Wangusi, alielezea kuwa hatua ya kuzima simu hizo, ambayo ilikuwa imeakhirishwa
mara tatu iliweza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo.
Tume hiyo haijashirikiana na kampuni za huduma
za simu kuzima tu bali pia simu ambazo wateja wake hawajasajiliwa.
Hatua hii imesababisha hasare kubwa kwa
kampuni za simu.
Hata hivyo tume ya CCK, imetenga bajeti ya
pesa itakazotumia kugharamia hasara ya kampuni za simu ingawa wateja wa simu
hizo hawatapata fidia yoyote.
Kampuni ya Safaricom, ambayo ina wateja
wengi zaidi ya kampuni zote za huduma za simu za rununu nchini Kenya, imezima
simughushi, 670,000 katika masaa 15 pekee.
Kampuni ya Airtel Kenya nayo imezima simu
100,000 huku yuMobile ikizima takriban simu 45,000. Kampuni ya Telkom Orange
imezima takriban simu 20,000.
Nani wa kulaumiwa kwa kuingiza nchini simu
bandia?
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment