Tuesday, October 2, 2012

Lori ya mafuta yapata ajali yaua 9 Mbeya... Koplo Mathias Joachim wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44 KJ Mbalizi Mbeya. Akishughulika. Upo juu kamanda lazima  uongezwe cheo mkuu wa nchi akikuona. Na: Charles Mwaipopo wa MALAFYALELEO-Blog, Mbeya. 

Macho ya mwandishi wa habari hii yameshuhudia miili tisa ikiwa imeungua vibaya na kutawanyika baada ya lori lililokuwa na mafuta linalosadikiwa ni mali ya kampuni ya LAKE OIL lenye namba za usajili T 814 BTC lililokuwa na tela ambalo kuungua vibaya.

Mwandishi wa habari hii anasema ajali hiyo imehusisha magari matatu, Lori lililokuwa likishuka taratibu mteremko wa Mbalizi na Hiace T 887 AHT linalofanya safari zake Mbalizi na Mwanjelwa sambamba na gari aina ya Ford Double Kibbin inayosadikiwa ni mali ya Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mary Mwanjelwa ambalo namba zake hazikupatikana mara moja kutokana na kuungua vibaya.

Shuhuda wa ajali hiyo Sadiki Nurdin amemwambia mwandishi wa habari hii kwamba lori lilikuwa likija kwa mwendo kasi hivyo alimshtua dereva wake na hivyo kulikwepa. 

Utingo huyo ameongeza kusema walipolikwepa lilianza kula ubavu wa gari lao na hatimaye lilikwenda na kukutana uso kwa uso na Hiace pamoja na gari linalosadikiwa ni la Mbunge wa Viti Maalum CCM na kusababisha maafa hayo. Mwandishi wa habari hii amesema kwa haraka haraka waliokufa ni 9, wawili kutoka kwenye Lori ambalo limelipuka na kusababisha maafa hayo, watu 6 kutoka kwenye basi la abiria aina ya HIACE, mpanda baiskeli, na mwendesha bodaboda. 

 Mwandishi wa habari hii anasema idadi ya majeruhi hajapata licha ya kwamba wamefikishwa katika hospitali ya Ifisi Mbeya Vijijini. Zoezi la uokoaji kwa mara ya kwanza limefanywa na Koplo Mathias Joachim wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania 44 KJ Mbalizi Mbeya.

Mashuhuda wa tukio hilo wampongeza sana Koplo huyo kwani ndiye aliyeweza pekee kuingia katika moto uliokuwa ukiwaka kwa nguvu katika ajali hiyo. 

No comments:

Post a Comment