Tuesday, July 24, 2012

Futari yetu ya leo,

Habari za asubuhi waungwana, tunaendelea na utaratibu wetu wa kuwaletea futari tutakayopika. Na hii ni kukuepushia usumbufu ewe mdau wa kidojembe, maana kufikiria cha kupika kila siku kwa muda wa mwezi mzima si kazi ndogo.

Leo nitapika futari ya kitanga, naam nimeamua kuwaletea vitu vya kitangatanga zaidi.

Tutaanza na ndizi mkono wa tembo (ndizi mbivu) za nazi, halafuta majimbi ya nazi, chapati na mbaazi za kulia chapati, samaki wa kukaanga na kachori. Uji uliopikwa kwa unga wa muhogo tia pilipili manga (black paper), chai ya mkandaa (black tea), halafu usisahau juice ya machungwa. Ukipata kipande cha parachichi (avocado) itakuwa vema, la umekosa pata kipande cha papai.

Nadhari hapo panatosha, ramadhan kareem.

No comments:

Post a Comment