Huduma katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea
kazini jana Jumatatu ya Julai 2, 2012.
Tathimini iliyofanyika
kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya
Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo.
Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.
Katika Idara ya watoto,
yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao
14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita
walikuja kazini ambapo watatu wako likizo.
Upande wa OPD yenye
Registrars saba, sita kati yao
walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja
kazini.
Idara ya Magonjwa ya
Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko
masomoni.
Upande wa Emergency
Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.
Kuhusu huduma za
upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za
huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani
hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..
KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA
KAZINI.
Imetolewa na;
Aminiel Buberwa
Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
No comments:
Post a Comment