Hosptali
ya AICC kuendesha kampeni ya kupima kisukari bure
24-07/2012
Arusha,
Tanzania.
Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kupitia hospitali yake ya AICC
kitaendesha kampeni ya kupima kisukari bure kwa wakazi wa Arusha ili kusaidia
wananchi kutambua kama wana ugonjwa wa kisukari au wapo katika hatari ya kuugua
ugonjwa huo.
Kampeni
hiyo itafanyika kesho (terehe 26-07-2012) katika hopitali ya AICC iliyopo
jijini Arusha ambapo madaktari wa hospitali ya AICC kwa kushirikiana na
madaktari wa wanaohudhuria mkutano wa Shirikisho la Madaktari wa Kimataifa
pamoja na madaktari kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania wataendesha
zoezi la upimaji huo.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa AICC, Bwana Elishilia Kaaya, amesema kuwa mbali na kupima
kisukari, madaktari hao pia watatoa ushauri wa namna bora ya kuishi na jinsi ya
kuzuia madhara ya kisukari kwa wale watakao kuwa wamekutwa na ugonjwa huo.
“Hospitali
ya AICC inatambua umuhimu wa afya za wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla
na ndio maana tumeona ni vema kufanya kampeni hii ya kupima kisukari. Napenda
kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa Arusha na vitongoji nyake kufika kwa
wingi kwani mbali na kupima pia itatolewa elimu na ushauri kutoka kwa wataalamu
hao.” alieleza Kaaya.
Kwa
mujibu Mkurugenzi Mwendeshaji, upimaji huo utaenda sambamba na mkutano wa
kwanza wa Shirikisho la Madaktari wa Kisukari wa Kimataifa ambao kwa mara ya
kwanza unafanyika hapa nchini. Mkutano huo utafanyika katika kituo cha AICC
ambapo madaktari wanaohudhuria mkutano huo na wale kutoka Chama cha Ugonjwa wa
Kisukari Tanzania watatoa huduma ya upimaji katika zoezi hilo.
“Tunaamini
baada ya kampeni hii wananchi watakuwa wamepata ufahamu juu ya hali ya afya zao
na kutumia vema ushauri wa madaktari kwa ajili ya kujikinga na kuzua athari za
ugonjwa huo”, alielezea Kaaya.
Mbali
na kuendesha kampeni hii, hospitali ya AICC imeanzisha kitengo maalumu cha
kisukari ambapo kila wiki madaktari hutoa huduma za matibabu na ushauri kwa
wagonjwa wa kisukri.
Ugonjwa
wa kisukari umekuwa ukiongezeka kwa kasi duniani ambapo taarifa za Shirika la
Afrya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2011 watu milioni 366
walikuwa wanaugua ugonjwa wa kisukari na mwaka 2030 idadi inakadiriwa kufika
milioni 552. Barani Afrika watu milioni 14 na nusu wanaugua ugonjwa huo huku
idadi ikitarajiwa kufika milioni 28 mwaka 2030 ikiwa ni ongezeko la asilimia 90.
No comments:
Post a Comment