Michel Platini, rais wa
shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA, amesema michuano ya Euro 2020 huenda
ikafanyika katika miji mbalimbali mwaka 2020, badala ya kuwa na mji mmoja ambao
utakuwa ni mwenyeji.
Utamaduni wa mashindano
hayo huwa ni nchi moja, au mbili, kushirikiana katika kuwa mwenyeji, kama
ilivyo wakati huu michuano hiyo kufanyika Poland
na Ukraine .
Mashindano yajayo
yatafanyika nchini Ufaransa, mwaka 2016.
"Euro 2020 inaweza
kufanyika popote barani Ulaya," alielezea Platini. "Yanaweza
kufanyika katika nchi moja yenye viwanja 12, au kufanyika katika uwanja mmoja
katika miji 12 au 13 ya Ulaya."
Platini ameelezea kwamba
wazo hilo pia
linaweza kuokoa senti katika kuepuka gharama kubwa za ukarabati, na juhudi za
kujenga viwanja vipya na kuimarisha viwanja vya ndege.
Uturuki ilitazamiwa na
wengi kupata nafasi ya kuandaa mashindano ya mwaka 2020, lakini ombi la nchi
hiyo limekumbwa na tatizo, kwa kuwa nchi hiyo pia ina nia ya kuandaa michezo ya
Olimpiki mjini Istanbul ,
mwaka huohuo wa 2020.
Mataifa ya Uskochi,
Wales na Jamhuri ya Ireland ,
rasmi pia yameelezea nia yao
ya kuandaa michuano ya 2020.
Platini ametangaza
kwamba uamuzi kamili utatangazwa kati ya mwezi Januari hadi Februari mwaka
ujao.
No comments:
Post a Comment