Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.Kifo
cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa
anajiandaa kupogania tena urais. Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara
kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika
hospitali moja mjini Accra
, Ghana .
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile
kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake. Kwa muujibu wa katiba
ya Ghana ,
Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi
hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68
alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.Hata hivyo hakuna maelezo
zaidi yaliyotolewa.Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema
kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya
Jumanne.Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana .
Chanzo: saidpowa blog
No comments:
Post a Comment