Hawa ni wapiganaji wa ITV Ufoo Saro na Monyo wakijiandaa kuvamia msitu katika ziara, si kazi ndogo.
Huyu ni dada Mariam wa Zenj FM akijiandaa nae kwa ziara asubuhi.
Baada ya kusubiri sana bila ziara kuanza muandishi mmoja akaanza kuigiza kama ndie mtaalam akionyesha watu mradi. Ndiyo raha ya waandishi hawakosi cha kupotezea muda mtacheka tu hata kama mmenuna.
Kituo kikuu cha mabus hayo yaendayo kasi kipo karibu na Kivukoni, hivyo leo nilijionea maajabu baada ya kuona vivuko viwili MV magogoni na MV kigamboni vikiwa katika upande mmoja kwa wakati mmoja. Kawaida vivuko hivi hupishana, kimajoa kikiwa kivukoni kingine kinakuwa kigamboni, nashangaa leo vyote vipo kwa pamoja...
Huyu ni meya wa jiji la Dar es salaam bwana Masaburi, ndie mwenyekiti wa mradi wa mabasi yaendayo kasi, nae tulikuwa nae katika ziara... Ni mtu mchangamfu sana, tena sana.
Baada ya kufika mchana mpiganaji mmoja wa ITV Ufoo Saro akaanza kuchoka.
Baada ya kufika saa nane mpiganaji mwingine wa gazeti la majira nae akawa hajiwezi taabani...
Hatimae safari ikafika mwisho, nikiwa na mpiganaji Frank, dakika za mwisho tukisubiri kusainishwa mishiko... hapa ni Blue Pearl Hotel iliyo katika jengo la Ubungo Plaza.
No comments:
Post a Comment