Majogoo wa jiji ama wekundu wa Anfield wameshusha kipondo cha mbwa mwizi kwa paka weusi Newcastle United kwa kuwabomoa bao 6-0 katika dimba la matakatifu James Park.
Matokeo hayo yamempa wakati mgumu kocha wa Newcstle Alan Pardew ukizingatia msimu huu sio mzuri kwake.
Machungu makubwa yamewapata Newcastle wakati kwa vijana wa Brendan Rodgers furaha na nderemo zimejaa usiku huu baada ya kufanya mauaji makubwa sana leo hii.
Mapema kabisa: Daniel Agger (katikati) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la mapema kwa Liverpool
Beki wa Nescstle Massadio Haidara akijaribu kuchukua mpira kutoka kwa nyota wa Liverpool Stuart Downing
No comments:
Post a Comment