Friday, April 19, 2013

Benki ya Dunia yaingia mkataba wa Bilioni 314 na Serikali ya Tanzania kusaidia miradi ya Umeme na gesi.


 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yapokea shilingi bilioni 314 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi ya Umeme, Gesi, Bajeti ya Serikali pamoja na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi ya gesi. Mkataba huo umesainiwa leo na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa Waziri wa fedha,  pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier  Mjini Washington DC. 
IMG_3784Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi. Susan Mkapa pamoja na wanasheria wa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini wakati Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakitia sahii mikataba hiyo.IMG_3792Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akipeana mkono na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier  mara baada ya kumaliza kutia saini mikataba hiyo. 
Picha na Ingiahedi Mduma na Eva Valerian – Washington DC

No comments:

Post a Comment