Wachezaji wa ASR Rabat wakicheza jaramba pembeni ya uwanja tayari kuenda kuongeza mashambulizi.
Katibu wa TFF Angetile Osiah wa kwanza kulia akizungumza na kocha msaidizi wa ASR Rabat Lahcen Ouadani (wa kwanza kushoto) katikati ni kocha mkuu wa ASR Rabat Abderazzak Khair. Ilibidi katibu wa TFF aingilie kati kuwa mkalimani kwani makocha hao wanazungumza kifaransa hivyo ilikuwa tabu kidogo wakati wa mkutano na wanahabari baada ya mechi kuisha.
Kocha wa ASR Rabat Abderazzak Kahir akimwambia kitu katibu wa TFF Osiah ili awaeleze wanahabari.
Azam FC imeshindwa kuutumia vema uwanja wa nyumbani baada ya
kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Wamorocco AS FAR Rabat katika pambano la kwanza kuwania
kuingia raundi ya tatu ya kombe la shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka
Shelsheli Azam walionekana kuchoka na kutumia muda mwingi kucheza pasi fupi
katika kipindi cha kwanza. Hali kadhalika wapinzania wao wakawa wamejaza viungo
wengi na mabeki ili kuhakikisha Azam hawapati bao hata moja.
Timu zote mbili zilipoingia kipindi cha pili zilicheza kwa
kukamiana hasa Azam FC walimtumia mshambuliaji wao hatari Gaudience Mwaikimba
aliyeingia kipindi cha pili kwa kupiga pasi ndefu na mashambulizi ya
kushtukiza.
Lakini mpaka mwamuzi huyo kutoka visiwa vya shelisheli anamaliza
pambano hilo si
Azam si ASR Rabat aliyeona lango la mwenzie hivyo Azam kutoka macho chini
kutokana na suluhu hiyo.
Na endapo Azam ingeshinda ingejiwekea mazingira mazuri ya kusonga
mbele hatua ya makundi ya michuano hiyo migumu barani Afrika. Kwa sasa Azam
watakuwa na kibarua kizito huko kaskazini mwa Afrika wiki mbili zijazo kwani
watahitaji ushindi tu na si vinginevyo.
Akiongea baada ya mechi hiyo kocha msaidizi wa Azam, Kalimangonga
Ongala alisema “Mechi ilikuwa ngumu lakini tulijitahidi kadiri ya uwezo wetu
kupata walau goli moja, lakini suluhu si mbaya kwetu kwani inatuma mwanya wa
kufanya mazoezi ya nguvu ili katika mechi ya marudiano tufanye maajabu.”
Kwa upande wake kocha wa ASR Rabat
Abderazzak Khairi amesema lengo lao lilikuwa ni kushinda lakini hali ya hewa ya
joto imewafanya wachezaji wake kuchea chini ya kiwango. Anategemea mechi ya
marudiano watacheza vizuri katika uwanja wa nyumbani.
Aidha aliongeza Azam ni timu nzuri na amefurahishwa na viwango vya
John Bocco na Gaudience Mwaikimba kwani walikuwa wakimnyima rah asana katika
dakika za majeruhi.
HAFIDH KIDO
20 Aprili, 2013
No comments:
Post a Comment