Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mgambo
Shooting na Yanga iliyochezwa jana (Aprili 17 mwaka huu) Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga imeingiza sh. 24,865,000 kutokana na watazamaji 4,386.
Viingilio katika mechi hiyo namba 162
iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 vilikuwa sh. 10,000 kwa
jukwaa kuu na sh. 5,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 5,547,337.50
wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,792,966.10.
Asilimia 15 ya uwanja sh. 2,820,680.08,
msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 90,000, waamuzi sh.
270,000, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 1,587,500.
Mgawo mwingine ni gharama za mechi sh.
1,692,408.05, Kamati ya Ligi sh. 1,692,408.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 846,204.05 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) sh.
658,158.69.
MAKOCHA AZAM, FAR RABAT KUTETA
Makocha wa timu za Azam, Stewart John Hall na AS
FAR Rabat ya Morocco ,
Abderazzak Khairi watakutana na waandishi wa habari kesho (Aprili 19 mwaka huu)
kuzungumzia mechi yao itakayofanyika Jumamosi,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Mkutano huo ambao pia utawahusisha manahodha wa
timu hizo mbili utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Barabara
ya Uhuru na Shaurimoyo.
Timu hizo zitakutana katika mechi hiyo ya kwanza
ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho itakayoanza saa 10 kamili jioni. Mechi
ya marudiano itachezwa nchini Morocco
wiki mbili baadaye.
JKT RUVU, YANGA KUUMANA JUMAPILI
Yanga ambayo inafukuzia kwa karibu taji la Ligi
Kuu ya Vodacom itapambana na JKT Ruvu katika mechi pekee ya ligi hiyo wikiendi
hii itakayofanyika Jumapili (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam .
Mbali ya mechi hiyo, nyingine zitakazochezwa
mwezi huu ni kati ya African Lyon na JKT Ruvu itakayofanyika Aprili 24 kwenye
Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam wakati Aprili 25 ni kati ya Ruvu Shooting na
Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam .
Nayo Coastal Union itaikaribisha Azam kwenye
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga katika mechi itakayochezwa Aprili 27. Uwanja
wa Taifa utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Simba na Polisi Morogoro
itakayofanyika Aprili 28.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
Aprili 18, 2013
No comments:
Post a Comment